Katika mkutano wa CES (Consumer Electronics Show) uliofanyika Las Vegas, Panasonic waja na luninga ya kustaajabisha iliyowavutia watu wengi kwenye mkutano huo.

panasonic-invisible-tv

Kama ilivyo kawaida kila mwaka watengenezaji wa vifaa vya umeme vinavyotumika katika maisha ya kila siku hufanya mkutano mkubwa maarufu kama CES, ambao mwaka huu mapema January ulifanyika katika jiji la starehe la Las Vegas huko nchini Marekani.

Mkutano huu ni wa kwanza kwa ukubwa ukiacha ule wa Barcelona unaofanyika kila mwaka kwa ajili ya maonyesho ya kampuni za simu. Kampuni ya utengenezaji wa vifaa vya umeme vya majumbani ya Panasonic ilitia fora kwa kutambulisha aina mpya ya Television (Luninga) ambayo ni ngumu kuitambua mpaka itakapowashwa.

Luninga hiyo iliyopewa jina la Invisible TV kutoka Panasonic ina uwezo wa kuongezeka urefu kulingana na matakwa ya mtumiaji. Pia katika kuhakikisha mtumiaji wa luninga hiyo hachoki kuitazama ni pale inapoweza kuwa kama kioo cha kabati na kuonyesha viombo vilivyomo kwenye kabati kabla ya kuwashwa.

Luninga hiyo ina uwezo wa kuonyesha video za kiwango cha hali ya juu (HD Videos) au picha za kiwango hicho bila shida. Ila kilichosikitisha wengi ni kwamba TV hiyon ilikuwa ni ya maonyesho tuu na bado haijangia katika soko rasmi.