Ikiwa na kamera yenye  12Mp, battery la 3000mAh, kioo cha inchi 5.2 na 4GB RAm HTC 10 inatarajiwa kukonga nyoyo za wapenzi wa smartphones katika Mwaka huu wa 2016.

htc-10

Kampuni ya HTC imeweka wazi toleo lake jipya la simu kwa Mwaka 2016, HTC 10 likiwa na maboresho ya baadhi ya mapungufu yaliyojitokeza katika toleo lililopita la simu hizo la kamera pamoja na battery. HTC walijitahidi kutengeneza kamera zao wenyewe za picha zenye 4 megapixel ili kuongeza mwanga Zaidi katika picha zinazopigwa lakini kamera hizo zilikuwa zinazalisha picha mbaya hasa wakati zinapopunguzwa (crop).

HTC wakaamua kuja na 20 megapixels ambazo hazikufanya vizuri hasa kwa picha za ndani na zile zinazopigwa karibu (indoors and closeups). Katika HTC 10 HTC wameamua kuweka uwiano sawa wa kamera, umbo pamoja na mziki ili kumpa mtumiaji wa kifaa hiki uhuru zaidi wa kukifurahia, inakuja na kamera yenye 12 MP kama kamera za matoleo mapya ya Samsung na iPhone.

1-htc-10-120416

HTC wamekuwa na mauzo mabaya hivi karibuni ukilinganisha na wapinzani wake Huawei pamoja na Samsung, kwa sasa kampuni ya HTC haipo miongoni mwa makampuni matano bora yanayotengeneza smartphones kwa sasa kama ripoti za Gartner shirika linalojihusisha na tafiti za simu linavyosema katika ipoti zake za hivi punde. Katika miezi ya hivi karibuni HTC walijikita zaidi katika kutengeneza vifaa vya mazoezi na Virtual Real.

Ikiwa imetangazwa leo (12.04.2016), lakini inatarajiwa kuingia sokoni hapo mwishoni mwa April japo bado bei ya simu hiyo haijawekwa wazi.

Kitu kingine cha muhimu cha kuangalia katika simu hii ni pamoja na battery yenye 3000mAh ambayo inakaa na chaji mpaka siku 2 kama kampuni hiyo inavyoahidi. HTC pia wameiongezea maradufu ubora kamera yake ya mbele (selfie Camera) kwa kuipa 5MP na kuifanya ifanane na zile za Apple pamoja na Samsung.

Katika umbo la nje simu hiyo limetengenezwa kwa chuma hivyo kuifanya iwe na shape nzuri kama kipande cha sabuni huku ikiwa inashikika vizuri mononi.