Kodi sio jina geni kwa wapenzi wa masuala ya burudani kupitia kwenye kompyuta zetu, hapo mwanzo ilifahamika kama XBMC (Xbox Media Center) na ni mbadala pekee kwa wapenzi wa kweli wa Windows Media Center.

Kodi-devices-smudged

Microsoft wameondoa Windows Media Center katika toleo lao la Windows 10 huku mamilioni ya wapenzi wa huduma hiyo wakiachwa njia panda. Kwa wale wa Windows 8 unaweza ukaupgrade kwenda kwenye Windows 8 Pro na kuinunua ila kwa wale wa Windows 10 haipo kabisa.

Hapa ndipo mbadala wa Windows Media Player anapohitajika, na hakuna mwingine zaidi ya Kodi kutoka XBMC Foundation. Kodi ni software ya bure ya kuplay (kucheza) Video, Audio, kucheza magemu, Picture pamoja na kustream Tv programs moja kwa moja kutoka katika kompyuta yako au simu yako yenye ubora wa hali ya juu kabisa katika soko la software kwa sasa.

Kodi inafanya kazi katika mifumo endeshi yote kama Windows, Linux, Mac OS, Android pamoja na iOS bila shida na inatumia 10-foot user interface kuangalia Tv moja kwa moja pamoja na kutumia remote control.

Kodi inakuja na bando au skins (muonekano) pamoja na plugin za kutosha zinazoweza kuplay video ya aina yoyote ile katika kompyuta au kifaa chako. Ikiwa imeandikwa kwa C++ kama programing language yake inaifanya Kodi kuwa kama framework ya kutengenezea application nyingine zinazotumika katika Smart Tv pamoja na home theater PC au katika Hotel Tevision System.

Ili Kodi iweze kufanya kazi katika mashine yako inahitaji kuwa na sifa zifuatazo:

  • Graphical Processing Unit yenye uwezo wa kucheza 3D
  • 4GB RAM inashauriwa Zaidi
  • 10GB Disk space

Music

Kodi inauwezo wa kuplay aina zote za mziki (music formats) kuanzia AAC, MP3, FLAC, OGG, WAV pia ina cue sheet, tagging support, MusicBrainz integration na smart playlist kwa ajili ya kucontrol mziki wako.

screenshot_pictures-800x450

Movies

Kodi inauwezo wa kuplay movie ya aina yoyote ile kuanzia zile za kustream online, ISOs, 3D, H.264, HEVC mpaka WEBM. Pia inatoa matrailer ya movie pamoja na makava yake.

Movies-example

Pictures

Katika upande wa pictures Kodi inauwezo wa kubrowse picture kutoka katika kila kona ya kifaa chako na kuamua mpangilio unaotaka bila shida yoyote ile.

screenshot_pictures-800x450

Kwa kifupi Kodi ni sehemu ya muhimu katika maisha ya kila siku ya mtumiaji wa kompyuta au simu za kisasa anayependa kupata kila kitu katika application moja.