Nadhani kila mtu anatamani kuwa na DSTV nyumbani kwake ili kufurahia vipindi vyenye radha tofauti kutoka katika channeli Zaidi ya 245 kutoka mataifa mbalimbai duniani, tatizo kubwa ni gharama kubwa inayotozwa na Dstv katika vifurushi vyake. Swahilitech tumeliona hilo na tumeamua kukusogezea Dstv kiganjani mwako.

dstv-mobile-android

Hakuna asiyejua ubora wa vipindi kutoka katika Channel za Dstv kwa wapenzi wa mpira, wapenzi wa music, wapenzi wa movie pamoja na wapenzi wa habari, maisha na dini.  Kwa kutumia njia hii unaweza kuangalia Zaidi ya channel 1000 kutoka duniani kote kwenye simu yako ya android au kwenye Laptop yako.

Ngoja tuende moja kwa moja kwenye pointi, tunaweza kuangalia channeli zote hizi kwa kutumia application inayoitwa Mobdro (Pongezi zote ziende kwa mtengenezaji wa application hii) ambayo haipatikani katika Google Play kwa sababu inakiuka baadhi ya sera za google.  Kwa kutumia application hii utaweza kuangalia channeli zote hizo zilizopangwa katika makundi (categories) kama ya Habari, Muziki, Tamthiliya, Movies, Michezo, Magemu, Teknolojia pamoja na nyingine nyingi tu. Kwa kuangalia hayo makundi unaona kila radha tunazopenda kuangalia katika TV zetu zinapatikana.

mobdro-02

Nitaorodhesha Channeli 5 katika kila kundi ili uweze kupata picha ya nini utakutana nacho katika application hii,

  • Habari; Angalia NBS, CNN, FOX NEWS, BLOOMBERG, SKY NEWS pamoja na Al-jazera bure katika simu yako
  • Shows; Angalia Adventure time, better call Call, community, regular show, family guy
  • Movies; Angalia Movies 24/7, HD Movies, All kinds of movies, Now playing, war movies bure katika simu yako
  • Michezo; Angalia ESPN, SKY SPORTS (1,2,3,4,f1), BT SPORTS 1 & 2, Liverpool TV, MUTV, Chelsea TV
  • Muziki; Angalia MTV hits UK, The Vault, D17, VEVO hits

Vitu vya kuzingatia kabla ya kuinstall Application hii;

  1. Simu ya Android yenye toleo la android kuanzia 2.5 na kuendelea.
  2. Internet
  3. Application ya Mobdro.

Njia za kufuata ili kuweza kuangalia DSTV Bure katika simu yako

-Download (pakua) Application ya Mobdro hapa na install katika simu yako. Kumbuka application hii haipo google pay store hivyo ni lazima uruhusu kuinstall application nje ya play store ili uweze kuinstall application hii. Fanya hivyo kwa kwenda kwenye settings–>Security–>Unknown Sources washa hapo. Kumbuka kuzima hii mara baada ya kuinstall application yako.

-Fungua application yako, kubali user agreement, alafu itakuletea kiwindow kisichokuwa na maandishi, click ok ili kupata version mpya ya application hii.

-Baada ya kumaiza kufanya installation, fungua application yako na taona category tofauti. Hapo utachagua Category na kuanza kuangalia bila tabu yoyote. (Zingatio: Ili kuweza kufurahia application hii ni lazima uwe na kifurushi cha data chenye MB za kutosha na mtandao wenye kasi nzuri kidogo).

Screenshot_2016-04-13-00-41-20

Nadhani utakuwa umefurahia Makala hii, ukiwa na tatizo lolote Tafadhali tuandikie kupitia sehemu ya maoni.