Leo tunajaribu kukuletea uchambuzi wa matoleo haya mawili ya simu yanayonunuliwa Zaidi katika hapa nchini kutoka kampuni ya Tecno ili kuweza kujua uzuri na mapungufu baina yao.

phantom5-vs-C8

Tecno imeendelea kusimama katika soko la smartphones kwa utoa simu nzuri tena kwa bei nafuu Zaidi ukilinganisha na makampuni mengine kama Samsung na HTC na inasemekana imechukua 50% ya soko la simu Afrika kwa sasa.

Katika matoleo yake ya hivi punde ya Tecno Phantom 5 na lile la Tecno Camon C8 inaonekana kampuni hii imeamua haswa katika kujikita katika uzarishaji wa simu za kisasa na zenye ubora sawa na ule wa makampuni makubwa ila kwa bei rahisi Zaidi.

Makala hii ina lengo la kukupa utofauti kati ya simu hizi mbili, kukuonyesha ipi imemzidi mwenzie katika lipi na kwa kiwango kipi ili kukuwezesha kufanya maamuzi sahihi pale unapotaka kuchagua moja ya simu hizi kutoka katika kampuni hii.

Tutaangalia vitu vifuatavyo katika kulinganisha matoleo haya mawili;

  • Ubora wa Kioo na picha zinazoonyeshwa
  • Mfumo wa simu nzima na Processor
  • 4G
  • Ubora wa Kamera
  • RAM
  • Diski Hifadhi
  • Uwezo wa kukaa na chaji
  • Bei

Ubora wa Kioo na Picha zinazoonyeshwa (Display Specifications)

Simu zote mbili zinatumia kioo chenye ukubwa wa inchi 5.5″, hii inamaanisha zina uwezo mzuri wa kuonyesha video pamoja na picha. Ukiondoa ukubwa, kuna tofauti kubwa katika uwezo wa kuonyesha, Tecno Phantom 5 ina kioo chenye resolution ya 1080 x 1920pixels kwa 400ppi pixel density. Wakati Tecno C8 ina kioo cheye resolution ya 720 x 1280 pixels kwa 267ppi. Pia zinatofautiana linapokuja suala la upana huku Phantom ikiwa nyembamba Zaidi 151×75.8×6.8mm wakati C8 ikiwa na 150×76.3×8.8mm.

Processor na Mfumo wa simu

Zote zinatumia mfumo endeshi wa Android 5.1 Lollipop, huku zikiwa na features zote za kubana matumizi ya betri na muonekano mzuri. Phantom 5 ikiwa na Processor ya Octa-core (8 cores) Cortex MediaTek processor ikiwa na mawimbi ya clock rate of 1.5GHz. Wakati C8 yenyewe ina processor ya 64-bit quad-core (4 cores) MediaTek MT6735 processor na Mali T720 GPU clocking at 1.3GHz. Hapa utaona Phantom ipo juu Zaidi kwani inaprocessor yenye uwezo mkubwa ukilinganisha na ule wa C8.

Uwezo wa kukamata 4G

Phantom 5 imekuja na uwezo wa kukamata mtandao wa kasi Zaidi wa internet wa 4G wakati C8 inakosa uwezo huu. Uwezo wa kukamata 4G katika matoleo ya Camon unapatikana katika Tecno Camon C5.

Ubora wa Kamera

Tecno Camon C8 ilitangazwa kama simu bora Zaidi kwa ajili ya picha kutoka kampuni ya Tecno huku ikiwa na 5MP kwa kamera ya mbele na 13MP kamera ya nyuma na zina Flash katika kamera zote ili kusaidia kupata picha nzuri katika mwanga hafifu.

Phantom 5 ina kamera ya nyuma yenye 13MP kama ile ya C8 akini ikiwa na 8MP kwenye kamera ya mbele hivyo kumuacha C8 mbali linapokuja suala la Selfie na simu za video.

RAM

RAM ni kigezo kikubwa na cha muhimu wakati wa kufanya manunuzi ya simu hasa simu za kisasa zinazorun application nyingi kubwa na nzito. Kwa sasa matumizi ya RAM kwenye simu hayatofautiani sana na yale ya kwenye kompyuta. Tecno Phantom 5 ina RAM yenye ukubwa wa 3GB wakati C8 ikiwa na 1GB, hapa unaona ni jinsi Phantom 5 imeandaliwa kwa ajili ya kupamabana na shughuli ngumu na nyingi ukilikganisha na C8.

Diski Hifadhi (ROM)

Kwa kuangalia tu utaona Phantom 5 ikija na diski hifadhi kubwa yenye uwezo wa 32GB wakati C8 ikiwa na 16GB na sehemu ya memory kadi yenye uwezo wa kwenda mpaka 32GB.

Uwezo wa kukaa na chaji

Hapa simu hizi zina uwezo sawa wa kukaa na chaji kwani zote zinakuja na betri lenye 3000mAh hivyo kuzifanya ziwe na uwezo Zaidi wa kukaa na chaji.

Bei

Bei ya Tecno Phantom 5 kwa sasa ni shilingi 840,000/= Tsh hii ni kwa mujibu wa bei katika maduka ya tigo, huku C8 ikipatikana mpaka kwa bei ya shilingi 270,000/= Tsh katika baadhi ya maduka.