Kampuni ya vifaa vya kisasa vya kidijitali iliyopo Hong Kong yatinga Afrika Mashariki. Simu hizo za kisasa zenye ubora wa hali ya juu sasa kupatikana Kenya Tanzania na Uganda kupitia kampuni mshirika iitwayo DESPEC.

ZURI_Smartphones

06 April 2016 – Watengenezaji wa Simu za kisasa aina ya Zuri(www.zuri.hk) pamoja na Mshirika na msambazaji wake DESPEC wamezindua simu hizo katika soko la Afrika Mashariki, yaani Kenya, Tanzania na Uganda.

Zuri ni bidhaa inayokua kwa kasi chini ya Kampuni iitwayo Amoli Group, ambayo ni wataalamu wa teknolojia waliobobea kwa zaidi ya miongo mitatu, na wamejitanua Ulaya, Mashariki ya Kati na Afrika katika vifaa vya kisasa vya kidijitali vikiwemo simu za kisasa, tablet, power banks na spika zisizotumia waya (Bluetooth speakers) na vinginevyo vingi. Zuri ilizinduliwa mwaka 2014 ikizingatia zaidi mahitaji yatokanayo na ukuaji wa kiuchumi wa tabaka jipya la wateja, katika uchumi ulioendelea na unaoendelea ambako, kutokana na ubora wake, Zuri itapokelewa na kukubalika zaidi.

Aina nne ya simu za kisasa za Zuri ambazo tayari zipo sokoni ni pamoja na C41, C46, C52 na S56, kila moja ina uwezo na ubora wakipekee wakutumia programu ya Android Kit Kat, laini mbili za simu, processors zenye kasi, kamera yenye ubora, kioo kipana, muundo na muonekano wa kisasa zaidi. C41 ina kioo cha inchi 4, processer ya quad core na 4gb memory; C46 ina kioo cha inchi 4.5, memory ya 8gb na camera ya 8megapixel; C52 ina kioo cha inchi 5, 8gb memory na 8mp camera; C56 5.5, processor ya octa core, 16gb memory na 13mp camera. Simu za Zuri pia zina waranti ya mwaka mmoja. Simu za toleo la awali zitakuwa na memory ya ziada ya 8mb, screen protector na kava zake.

“Zuri imetengenezwa “kwa ajili yako” kwa maana halisi Zuri imekupa wewe kipaumbele” hayo yalisemwa na Vikash Shah Mkurugenzi Mkuu wa Zuri. Ni kauli iliyowazi kabisa juu ya utendaji na ushirikiano wetu na wateja. Tunaweka mahitaji na vipaumbele vya mteja kwanza katika kila jambo tunalolifanya.”

“Sasa hivi watu takribani bilioni moja duniani kote wanatumia simu za kisasa na tunalenga wengine bilioni moja,” aliendelea Vikash Shah. “Hawa wanaojiunganisha wapya tunawaita ‘wateja wapya wa simu za mkononi’. Hawa wateja wako kila mahali kuanzia familia inaponunua simu mpya, mwanafunzi anapouza komputa yake ya mezani kwa ajili ya simu ya mkononi, mpaka mfanyabishara mdogo anayetaka kuwasiliana na wateja wake.”

Eneo la Afrika Mashariki linakua kwa kasi katika matumizi na ununuaji wa simu za aina ya smartphone, na idadi inazidi kuongezeka. Ripoti kutoka IDC imebaini kuwa katika simu za mkononi zilizoingia Afrika mwaka 2015, inakisiwa kuwa nusu yake ni aina ya smartphone na idadi inatarajiwa kuongezeka kufikia asilimia 80% katika kipindi cha miaka mitano ijayo. Kwa hiyo Zuri imejipanga kulikabili soko hili ikiwa na bidhaa inayokidhi mahitaji ya mteja.

Vikash Shah alieleza: “Afrika Mashariki inatoa fursa ya Zuri kukua, kutokana na mahitaji ya simu za kisasa aina ya smartphone. Tuna uhakika kabisa DESPEC watatufikisha katika soko la Kenya, Tanzania na Uganda. Zuri tumejizatiti kuhakikisha uwepo wetu katika Afrika Mashariki, na DESPEC ndiye mshirika wakipekee atakayefanikisha hili.

Riyaz Jamal, Mkurugenzi Mkuu wa DESPEC, alisema: “Tuna furaha kubwa kuongeza simu za kisasa za Zuri kama moja ya bidhaa zetu, na tunaimani kuwa Zuri itakuwa na maisha marefu Afrika mashariki. Wauzaji na wateja wanahitaji simu ya kisasa iliyo tofauti na zingine zote. Tunaamini kuwa Zuri ni bidhaa yenye ubora na muundo wa kipekee utakao tuwezesha kufanya biashara Kenya, Tanzania na Uganda.”

Vikash Shah aliendelea kusema: “Mpango wa Zuri ni kutoa njia rahisi, sahihi na imara za mawasiliano duniani.Uwezo wetu na utaalamu wa hali ya juu katika utengenezaji wa bidhaa zetu zinatoa uwiano kati ya thamani na utendaji wake kwa mtumiaji.”
Tunatarajia wasambazaji na wauzaji wa jumla na reja reja katika Afrika Mashariki wataelezea faida zitokanazo na Zuri kama bidhaa inayoendana na malengo yetu.” Shah aliongeza.

Kuhusu Zuri:
Zuri ni mtengenezaji na muundaji wa simu za kisasa za mkononi (smartphones), tablets, na vifaa vya kisasa vya dijitali. Makao makuu yake yako Hong Kong, kampuni hii hufanyakazi na wabia wa mashirika mbalimbali ulimwenguni kuhakikisha wanazalisha bidhaa bora iliyosukwa kuendana na thamani ya fedha ya mteja.
Fahamu zaidi kuhusu Zuri katika www.zuri.hk