Apple wamesitisha kutoa updates za QuickTime katika matoleo yanayotumika katika mfumo endeshi wa Windows hivyo kuongeza hatari ya wadukuzi kupata mwanya wa kudukua kompyuta za watu wanaotumia huduma hiyo.

quicktime

Kampuni ya Apple kwa sasa imesitisha kutoa updates katika software yao maarufu inayotumika kuplay music na kuangalia matrailer ya muvi katika tovuti yao. QuickTime player ni software inayotumika sambamba na iTunes katika kompyuta zinazotumia mfumo endeshi wa Windows.

Kwa mujibu wa kampuni inayojihusisha na ulinzi na usalama wa mitandao ya Trend Micro imesema Apple hawana mpango wa kutoa updates za software hiyo isiyokuwa na watumiaji wengi kwa sasa hivyo kuongeza mwanya wa wadukuzi kuvamia kompyuta za watumiaji wa software hiyo kwa kuwa hazipati tena updates za kuzuia mianya ya wadukuzi.

Trend mpaka sasa wamegundua mianya miwili inayoweza kutumika na wadukuzi kuleta madhara katika kompyuta za windows kupitia software hiyo. Mianya hiyo haitazibika na kadri siku zinavyozidi kwenda mianya zaidi itaongezeka kwa kuwa hakuna updates kutoka kampuni hiyo.

Hivyo unashauriwa kama unatumia software hiyo ni bora ukaitoa ili kupunguza uwezekano wa kudukuliwa na wadukuzi. Trend imesema mianya iliyogunduliwa haiwezi kuidhuru kompyuta moja kwa moja ila kuna uwezekano mkubwa wa wadukuzi kutumia mianya hiyo kupitisha malware.

Unistall program hii kwa kwenda kwenye Program and features katika Control Panel kisha chagua QuickTime alafu bonyeza uninstall.