Kampuni ya Kichina ya kutengeneza vifaa vya umeme ya PiPO imetoa toleo la pili la kompyuta zake ndogo zenye umbo la keyboard huku zikiwa na Windows 10 kama mfumo endeshi.

pipo-kb1

Ikiwa inatumia processor ya Cherry Trail, battery ya 2500mAh na RAM ya 4GB au 2Gb PiPO KB2 ni kompyuta tosha inayojitegema ikiwa na umbo dogo zaidi la keyboard inayoweza kujikunja.

Katika kongamano la kibiashara linaloendelea huko HongKong kampuni ya PiPO imetambulisha rasmi bidhaa hiyo mpya ambayo itaingia rasmi sokoni hapo mwezi wa tano.

pipo-kb2-03_story

PiPO KB2 itakuwa na Processor ya Intel Atom x5-Z8300 (Cherry Trail processor) yenye uwezo wa 1.84GHz huku ikiwa na Graphic Card ya Gen8. Kompyuta hiyo ndogo itakuwa na RAM ya 2GB au 4GB huku ikiwa na diski hifadhi yenye ukubwa wa 32GB au 64GB kulingana na toleo itakuwa msaidizi mkubwa sana kwa wapenda kompyuta ndogo.

pipo-kb1-02_story

Kwa mujibu wa Notebook Italia kifaa hicho kitakuwa na sifa zote za kompyuta za kisasa kama Port za USB 3, WiFi, Audio Jack, Bluetooth pamoja na microSD Card slot. Bei ya Notebook hiyo haijajulikana mpaka sasa japo inasemekana itakuwa na bei nafuu kidogo.

PiPO itakuja na Windows 10 Home Edition ikiwa installed kwenye kompyuta hiyo, tofauti na toleo la kwanza la PiPO KB1 ambalo lilikuwa kubwa na lisilokunjika.