Katika toleo jipya lililotoka katika siku za karibuni (latest update) facebook wameleta huduma itakayomwezesha mtumiaji wa messenger kupiga simu za makundi (Group Calls).

Facebook-Messenger-group-call

Katika huduma hiyo mpya mtumiaji wa messenger anaweza akapiga simu kwa watu wote wa kundi analochati nalo kwa wakati mmoja. Kitu ambacho mtumiaji wa application hiyo anatakiwa kufanya ni kutengeneza group (kundi) la watu anaotaka kuchat nao na kubonyeza kitufe cha kupiga simu akiwa ndani ya group. Unaweza ukachagua nani simu mfikie na nani simu hiyo haimuhusu katika screen inayofuata baada ya kubonyeza kitufe cha kupiga.

Ripoti kutoka katika mtandao wa The Verge zinasema mtumiaji wa messenger anaweza akapiga simu mpaka kwa watu 50 kwa pamoja kwa kutumia huduma hiyo. Huduma hiyo kwa sasa inapatikana katika matoleo ya messenger ya Android na iOS.

Mtandao huo mkubwa wa kijamii duniani unaboresha application yao ya mesenger kila kukicha na kuifanya kuwa application bora kabisa ya kuchat ikiwa na watumiaji milioni 900 duniani kote.