Google imeongeza huduma tatu katika application yake ya Inbox by Gmail inayomuwezesha mtumiaji wa huduma hiyo kufanya mambo mengi zaidi ya kutuma na kupokea email katika application hiyo.

Inbox-by-Gmail

Inbox by Gmail sio jina geni kwa watumiaji wa huduma za barua pepe kutoka google, kitu cha msingi cha kufahamu hapa huduma hii ni tofauti kabisa na ile application ya Gmail tuliyoizoea katika simu zetu inayotuwezesha kutuma na kupokea barua pepe.

Inbox by Gmail inamuwezesha mtumiaji wa huduma hiyo kupokea barua pepe, kuzipanga katika kalenda kulingana na matukio yaliyomo katika barua pepe hiyo, kujibu au kulipia baadhi ya huduma kupitia application hiyo.

Fikiria umepokea barua pepe kutoka katika kampuni ya huduma za matangazo ya televisheni kama DSTV ikikukumbusha malipo ya mwezi huo. Ukiwa katika application ya Gmail utaweza tu kusoma barua pepe hiyo au kutoa nakala yake (print), hii ni tofauti katika application ya inbox by gmail kwani utaweza kulipia moja kwa moja kwa kutumia application hiyo au kuitunza katika Google Kalenda kama kumbukumbu.

Ni vizuri kuinstall application hii ili uweze kuifahamu zaidi. Kwa sasa kuna huduma tatu zimeongezwa na google katika app hii ambazo ni;

1. Streamlined events:Kwa sasa Gmail itamuwezesha mtumiaji kufuatilia matukio muhimu anayotumiwa kwenye barua pepe zake moja kwa moja.

2. Glanceable Newsletters: Kama ilivyokuwa katika application ya Gmail, newsletters zilikuwa na tab ya peke yake ili kumpa msomaji wa barua pepe urahisi zaidi wa kusoma barua pepe za msingi. katika update hiyo inbox itakuwa inapanga newsletters kulingana na umuhimu wake (priority) na itajikita zaidi katika linki za newsletter hizo.

3. Saved links: Kwa sasa watumiaji wa Inbox wataweza kuhifadhi (save) linki zao na kushare na watu wengine pale wanapotaka.

Ili kuweza kupata application hii kutoka Google unaweza ukaidownload moja kwa moja kutoka katika Playstore kama wewe ni mtumiaji wa Android.