India imepanga kujenga Treni yake ya kwanza ya mwendo kasi itakayokuwa inapita chini ya bahari ili kuunganisha miji ya Mumbai na Ahmedabad gazeti la The Economic Times limeripoti.

Bullet-Train

Safari kati ya miji hiyo miwili ya kibiashara itachukua masaa mawili kwa Treni hiyo itakayokuwa ikisafiri kwa mwendokasi wa 350 km/h, tofauti na hali ilivyo sasa kwa kutumia Treni ya Duronto Express  safari hiyo huchukua zaidi ya masaa saba.

Umbali kati ya miji hiyo miwili ni kilomita 508 na kilomita 21 za reli ya treni hiyo zitapita chini ya bahari. Ujenzi wa Treni hiyo utadhaminiwa na serikali ya Japan kwa 80% huku serikali ya India ikitoa kiasi kilichobakia na ujenzi unatarajiwa kukamilika mapema mwaka 2018.