Kampuni ya kutengeneza simu ya kichina ya Le Eco imeachia matoleo matatu ya simu za kisasa maarufu kama smartphones juzi mjini Beijing.

le-2-pro-

Katika matoleo hayo ya smartphones kutoka kwa Le Eco watupilia mbali kitundu cha kuchomeka earphones (audio jack) na kuamua kuja na teknolojia ya USB C huku ikiwa na teknolojia ya CDLA (Continual Digital Lossless Audio) ambayo inasemekana kutoa audio yenye kiwango cha hali ya juu ukilinganisha na zile za headphone Jack.

Katika matoleo yote matatu kampuni hii imeamua kuyapa kava la chuma huku wakiongezea utamu zaidi kwa kuweka fingerprint scanner kwa ajili ya usalama zaidi. Simu hizi zote zinatumia mfumo endeshi wa Android 6.0 Marshmallow OS huku ukiwa umeongezewa mbwembwe na kampuni hii ili kuendana na simu zake katika tabaka la juu.

le1

LeEco Le 2 inauzwa kwa bei ya shilingi 400,000 sawa na Yuan 1,099 na Le 2 Pro ikiuzwa kwa bei ya shilingi 550,000 sawa na Yuan 1,499 wakati Le Max 2 inauzwa kwa bei ya Yuan 2,099 sawa na shilingi 740,000 za kitanzania kwa toleo lenye RAM ya 4GB na diski hifadhi ya 32GB.

Simu ya Le 2 inakuja na kioo chenye ukubwa wa inchi 5.5 huku ikiwa na processor ya Helio X20 tri-cluster deca-core processor huku ikiwa na RAM ya 3GB na diski hifadhi ya 32GB. Ina kamera ya 16MP katika kmera ya nyuma huku ikiwa na 8MP katika kamera ya mbele.

Simu hiyo inakuja na betri lenye uwezo wa 3000mAh ikiwa na uwezo wa kuchajiwa kwa haraka zaidi, kwa upande wa Network simu hii inakuja na WiFi 802.11ac, 4G LTE na VoLTE.

Screenshot (1)

Hizo ni baadhi ya sifa za simu hii ya chini kabisa katika ubora kati ya hizo tatu zilizotoka. Kwa sasa simu hizi bado hazijaanza kutoka nje ya China na pale zitakapoingia Tanzania swahiliTech tutakuwa wa kwanza kukuletea orodha ya maduka yanayouza simu hizi za kisasa na za kiwango cha juu kabisa ukilinganisha na bei yake.

le4

le 10