Leo tunakuletea uchambuzi wa matukio pamoja na viwango tofauti vinavyohusiana na Mfumo endeshi unaomilikiwa na kampuni ya Alphabet kutoka Google ambao kwa sasa unaongoza kutumika katika simu duniani.

1.16-billion

Idadi ya simu zilizoingizwa sokoni mwaka 2015 zikiwa zinatumia mfumo wa Android, hii ni kwa mujibu wa wataalamu wa tafiti Gartner. Hiyo ni karibia 82% ya soko lote la simu huku iOS ikiwa na simu milioni 225.85.

1.37-billion

Kiwango cha smartphones zinazotarajiwa kuingia sokoni zikiwa na Mfumo endeshi wa Android kama Gartner walivyotabiri. hiyo itakuwa 84% ya soko lote la simu duniani.

74.9-billion

Mapato yaliyopatikana katika kampuni ya Alphabet inayomilikiwa na Google kwa mwaka 2015, huku ikiwa imepata faida ya bilioni 15.8.

2005

Mwaka ambao kampuni ya Google iliinunua Android kutoka kwa kampuni ya Android Inc. iliyokuwa ikimilikiwa na mmoja wa wahandisi wa zamani wa Apple bwana Andy Rubin. Kabla ya hapo Android ulikuwa mfumo endeshi wa kamera na baadhi ya vifaa vidogo vidogo.

2008

Mwaka ambao mfumo endeshi wa Android uliingia sokoni rasmi kama mfumo endeshi wa simu unaomilikiwa na Google, huku ukiwa na huduma nyingi za google ndani yake kama gmail, kalenda na play store. Android version 1.0.

2009

Mwaka wa Android CupCake, kama unavyojua mfumo endeshi wa Android huwa unatumia majina ya vyakula katika matoleo yake. Haya ni baadhi ya majina yaliyowahi kutumika katika mfumo endeshi huo Donut, Eclair, Froyo, Gingerbread, Honeycomb, Ice Cream Sandwich, Jelly Bean, KitKat, Lollipop na sasa wana Marshmallow.