Ule mpambano mkali wa kugombania soko kati ya mabepari wawili wa smartphones Samsung na Apple umeingia katika sura mpya huku safari hii Samsung akionekana kuibuka kidedea katika matoleo ya hivi karibuni.

iphone6-vs-S7

Mwaka jana tulishuhudia kuachiwa kwa Apple iPhone 6s simu ambayo ilibadilisha sana soko la smartphones na kuwafanya Apple waongoze kimauzo. iPhone 6 ilikuja na teknolojia ya Fingerprint Scanner kwa mara ya kwanza huku ikiwa na kamera nzuri kabisa kutoka Apple. kimuonekano simu hii ilikuwa kila kitu kwa mtumiaji wa simu wa kawaida.

Mwanzoni mwa mwaka huu katika mkutano mkuu wa watengenezaji wa simu uliofanyika huk Barcelona, Uhispania kampuni pinzani ya Samsung ilitambulisha rasmi toleo lake jipya la simu za Galaxy S7 na Galaxy S7 Edge. Tangu kutambulishwa kwake simu hizi zimekuwa zikifanya vizuri sokoni huku takribani watu milioni moja walikuwa wameweka order kabla hazijaingia sokoni.

Leo tunajaribu kuzichambua simu hizi kwa kuangalia uwezo wa kila mojawapo katika baadhi ya vitu vya msingi ambavyo watumiaji wa simu wamekuwa wakitupia macho.

Samsung Galaxy S7 Vs Apple iPhone 6s

1. Kamera

Samsung Galaxy S7 imeipeleka teknolojia ya kamera katika level nyingine kabisa, ikiwa na Dual Pixel kamera na aperture ya f/1.7 inakuwa kamera nzuri kabisa kuwahi kutokea katika smartphones. Huku iPhone ikiwa na kamera yenye aperture ya f/2.2. Aperture ni kiwango cha mwanga kinachoruhusiwa kuingia kwenye kamera. Kwa kuangalia kigezo cha aperture utaona S7 inaruhusu kiwango kingi cha mwanga kuingia kwenye kamera na kupelekea kuzalisha picha nzuri kwenye mazingira yote ukilinganisha iPhone 6.

2. Display

Samsung siku zote wanaongoza kwa kutengeneza vioo vyenye muonekano mzuri. Hii imepelekea hata baadhi ya makampuni pinzani ya simu kutengenezewa vioo na Samsung wakiwepo Apple wenyewe kwa kipindi fulani hapo nyuma na wanampango wa kuendelea kutumia vioo kutoka Samsung kuanzia mwaka 2018 kama habari kutoka katika baadhi ya vyanzo zinavyosema.

Muonekano wa Super AMOLED screen ni mzuri zaidi ukilinganisha na ule wa IPS LCD unaotumika kwenye iPhone 6. Pia kwenye resolution S7 ina resolution ya 2560×1440 na Quad HD resolution ikiwa imeiacha mbali iPhone 6 ambayo ina resolution ya 1334×750.

3. Water and dust resistance (uwezo wa kuzuia maji na vumbi)

Kitu kikubwa ambacha kampuni ya Samsung inaonekana kutamba nacho katika kila tangazo la S7 ni uwezo wake wa kukaa ndani ya maji kwa dakika 30 kwenye maji yenye kina cha mita 1.5 na ikiwa imepewa IP68. Hivyo unaweza ukaenda kuoga na S7, au ukatoka nayo kwenye mvua bila shaka. Ila hali ni tofauti kabisa kwa iPhone 6s kwani utapata hasara.

4. Diski Hifadhi

Apple wameendelea na msimamo wao wa kutumia 16GB kama kiasi chao cha diski hifadhi cha kawaida japo unaweza ukaongeza mpaka kufikia 128GB. Hali ni tofauti kwa S7 wao wameamua kuanzia 32GB ambazo unaweza ukaongeza mpaka kufikia 200GB.

5. Dual-SIM (Laini 2)

Siku hizi sio jambo geni kumuona mtu akiwa na laini zaidi ya moja katika kutafuta unafuu wa mawasiliano na vifurushi vya kuperuzi hasa katika nchi za ukanda wetu wa Afrika. Samsung wameliona hilo na kuamua kuleta toleo la laini mbili la S7 hivyo kukufanya usiwe na ulazima wa kutembea na simu mbili kila unapoenda. Hii ni tofauti kabisa kwa iPhone ambao bado hawajatoa simu ya laini 2.

6. RAM

Samsung S7 inakuja na RAM ya 4GB huku iPhone 6s ikiwa na RAM ya 2GB.

7. Battery

Moja ya vitu vinavyolalamikiwa zaidi katika simu za kisasa (smartphones) ni battery, iPhone 6s inakuja na battery la kinyonge zaidi ukilinganisha na mfumo wenyewe wa iOS lenye 1715mAh tofauti na Samsung S7 yenye 3000mAH.

Pamoja na yote hayo bado Apple iPhone 6s ni simu nzuri sana hasa linapokuja suala la usalama wa data za mtumiaji na usalama wa kifaa chenyewe. Uwepo wa iOS 9 kama mfumo endeshi unaotumika katika simu hizi kunaipa boost kubwa sana kwa sababu mfumo huu endeshi bado ni mfumo bora kabisa kuwahi kutumika katika simu.

Bado tunaisubiri kwa hamu simu mpya ya iPhone 7 ambayo inasemekana itatoka mwezi wa tisa mwaka huu ili kuweza kuona nini kipya Apple watatuletea sisi mashabiki wa smartphones kutoka kwenye kampuni hizi mbili.