Soko la simu za mkononi limetoka mbali sana hasa ukiangalia miundo na teknolojia za simu kutoka katika simu za mkononi zenye miito ya polyphonic, kutoka kwenye vioo vya kawaida mpaka kwenye vioo vya rangi vyenye uwezo  mkubwa, kutoka kwenye batani mpaka kwenye vioo mguso.

Yotaphone2

Japokuwa kuna mabadiliko makubwa sana katika uundaji wa simu kuanzia miaka ya 2010, kuna simu zimezidi kuwa za kipekee sokoni na hakuna anayeweza kuzifananisha na nyingine.

Makampuni yanayotengeneza simu wanajaribu kuwa wabunifu zaidi ili kuwashangaza watumiaji wao kila siku toleo jipya linapotoka. Kuna wengine wanaongeza vitu ambavyo vinaonekana si vya kawaida japo kuna wengine wanaongeza vitu vinavyoibua hisia kubwa miongoni mwa wapenzi wa simu zao.

Leo tutaangalia matoleo ya simu kali zaidi duniani ambazo zina vitu ambavyo huwezi kuvipata katika simu nyingine yoyote ile.

1. Motorola X force – Shatterproof display (Kioo kisichovunjika)

MotoX-Force-01

Katika simu za siku hizi kioo kimekuwa kitu cha kwanza kuharibika kabla hata ya betri la simu kufa, hii inatokana na ukubwa wa vioo na teknolojia za vioo vinavyotumika katika simu. Motorola waliliona hilo na kuamua kuja na toleo la simu linalotumia teknolojia kali zaidi na kukifanya kioo cha simu ya Motorola X Force kuwa simu ya kwanza duniani yenye kioo kisichovunjika.

Kioo cha simu hiyo inasemekana kina matabaka matano (layers) yaliyotengenezwa kwa vitu tofauti vinavyosaidia kuzuia mvunjiko pale simu inapogongwa au kuangushwa.

2. Jupiter IO 3 – Smokable Phone (Simu yenye Inayovutika kama sigara)

Jupiter-vapouriser-smartphone-03

Kampuni ya kimarekani inayotengeneza simu hizi ya Vaporcade imejribu kuleta kitu kipya katika soko la smartphones kwa kukuletea simu zinazovutika kama sigara au maarufu kama e-cigarette. Simu ya Jupiter IO 3 inakuja na batani inayokuwezesha kuongeza kiwango cha joto unalotaka litoke kwenye sigara yako huku kukiwa na battery maalumu inayokusaidia kufanya hivyo. Juu simu hiyo kuna kitundu kinachokuwezesha kuweka radha ya sigara unayotaka kama ni Sweet Menthol au la na kukupa radha ile ile kama unavuta sigara halisi.

3. LG G5 – Modular Phone (Simu ya Vipande Vipande)

LG-G5-08

LG G5 imekuwa simu ya kwanza ya vipande vipande duniani, kampuni ya LG wameipiku kampuni ya Google ambayo kwa muda sasa bado wanafanya utafiti juu ya kuleta simu za aina hii. LG G5 ni simu pekee ambayo unaweza ukaitengenisha kwa vipande vipande na kuiunga tena bila tabu.

4. Sony Z5 – 4K display (Kioo cha 4K)

Sony-Z5-01

Kuweka pixels nyingi per inch resolution kunaifanya simu hii kuwa simu ya kwanza duniani kuwa na teknolojia ya hali ya juu ya video ya 4K. Video za 4K ni video zenye ubora wa hali ya juu kabisa duniani kwa sasa. Kioo cha ichi 5.5 kilichowekwa kwenye simu hii kinamfanya mtumiaji wa simu hii kufurahia video zaidi.

5. Saygus V Squared – Two microSD card slots (Sehemu 2 za kuweka Memory Card)

Saygus-V-Squared

Unaujua umuhimu wa kuwa na nafasi ya kutosha katika simu? Kampuni ya Saygus kutoka Marekani wao wameamua kuja na simu yenye uwezo wa kuweka Memory Card mbili zenye uwezo mpaka 200GB ukiacha ule uwezo wake wa ndani wa 64GB. Simu hii haishii hapo pia ina fingerprint scanner pembezoni mwake.

6. LG V10 – Dual front screen (Vioo viwili mbele)

LG-V10

Simu hii ina vioo viwili kwa mbele ikiwa na kimoja kwa ajili ya kuonyesha taarifa kama za hai ya hewa, muda pamoja na saa na kinafahamika kama e-ink screen, wakati kingine kitumika kwa matumizi mengine ya simu. Kioo cha e-ink muda wote huwa kinaonyesha hivyo kumrahisishia mtumiaji wake.

7. Yotaphone 2 – Screen at the back too (Kioo upande wa nyuma)

Yotaphone2

Yotaphone 2 ndio simu ya kwanza inayotumia mfumo endeshi wa android yenye kioo nyuma. Kioo hicho cha e-ink kimeenea eneo lote la nyuma la simu hiyo na kumuwezesha mtuiaji wake kukitumia kwa kutuma na kupoka message, kuvinjari katika mitandao ya kijamii na shughuli nyingine ndogondogo pale battery la simu linapokuwa chini.

8. Samsung Galaxy S7 Edge – Curved Edges (Kioo chenye ncha zilizojikunja)

Galaxy-S7-edge

Kioo chenye ncha zilizokunjika kwa mara ya kwanza kinaonekana katika matoleo ya simu za Samsung S7 Edges na kinaongeza vionjo katika simu hii.

9. Blackphone 2 – 100% encryption

Blackphone2

Simu hii inayoendeshwa na mfumo endeshi wa Silent ukiwa juu ya android imelenga zaidi katika kumpa mtumiaji wake usiri wa kutosha kwa kumwezesha ku-encrypt kila kitu kinachoingia katika simu hii. Simu hii imetengenezwa maalumu kwa ajili ya watu wanaopenda usiri au makampuni yanayopenda usiri zaidi.

10. Oppo F1 Plus – 16 MP front camera (Kamera ya mbele yenye 16 MP)

Oppo-F1-Plus

Kampuni ya Oppo imeamua kuwafurahisha wapenda selfie kwa kuwaekea kamera ya mbele yenye uwezo mkubwa zaidi katika simu kwa sasa 16MP. Tofauti na simu nyingine simu hii ina kamera ya nyuma yenye uwezo mdogo zaidi ya ule wa kamera ya mbele, 13MP.

Usisahau kulike page yetu ya Facebook kwa habari, makala na uchambuzi zaidi.