Hali ya usiri wa taarifa za watumiaji wa mtandao duniani kote imekuwa ya kutilia shaka zaidi kwani kwa mara ya kwanza watumiaji milioni 1 wa mtandao mkubwa wa kijamii wa Facebook wanatumia kivinjari (browser) cha TOR ili kulinda taarifa zao.

Tor-browser-facebook

Facebook wamesema watu wanaotumia kivinjari cha Tor kuingia katika mtandao huo wameongezeka hadi kuvuka milioni 1 mwezi April mwaka huu. Hii ni kwa mara kwanza kivinjari hicho kufikisha idadi ya watu hiyo ya watu katika mtandao huo.

Kivinjari cha Tor, maarufu kama onion router kinafahamika kwa kutoa usalama wa taarifa za mtumiaji anapokuwa anatembelea tovuti mbalimbali mtandaoni. Tor inazuia watu wengine mtandaoni kukufahamu eneo ulipo, kifaa unachotumia na baadhi ya taarifa unazotafuta mtandaoni hivyo kukufanya kuwa salama wakati unavinjari.

Tor pia inaficha kila kitu unachofanya au mawasiliano unayoyafanya mtandaoni ili kuweza kulinda usiri wako. Kabla ya hapo ilikuwa ni ngumu kidogo kuingia Facebook kwa kutumia kivinjari hiki kinachopigwa vita na mashirika ya usalama kama NSA na CIA, kwa sasa Facebook wametengeneza mlango wa kuingilia katika kivinjari hiki ili kurahisisha matumizi ya Facebook kwa kutumia Tor.

Watu wengi hupenda kutumi Tor kwa sababu ya uwezo wake wa kubadilisha eneo ulipo, uwezo wa kuficha mawasiliano na uwezo wa kuzuia wafuatiliaji wa mambo ya usalama.

Kupakua kivinjari hiki tumia linki hii “Pakua TOR Browser”