Kampuni ya kutengeneza vifaa vya ujenzi yenye makao makuu yake nchini Marekani imeoa toleo lake la kwanza la smartphone “MD501” hivi karibuni ikiwa na muonekano imara zaidi.

Dewalt-MD501-smartphone

Simu hiyo yenye kioo mguso (touch screen) inaweza kutumika hata kama mtumiaji amevaa gloves na ina uwezo wa kustahimili joto mpaka digrii 60.

Simu hizo zikiwa zimetengenezwa na kitengo cha utengenezaji simu cha kampuni hiyo cha Global Mobile Communications ina 4G , kamera 13MP, processor ya 1.3GHZ  RAM 2GB, Kioo cha ichi 5 na betri la 3,950mAh huku ikiwa na uwezo wa kuchaji kwa Wireless. Simu hiyo inatumia mfumo endeshi wa Android 5.1 (Lollipop).

Dewalt pia wametengeneza loud spika yenye kiwango itakayomwezesha mtumiaji kuitumia hata katika maeneo y site yenye kelele nyingi.