Inasemekana kampuni ya kutengeneza software ya Microsoft inaajiri wataalumu kutoka katika kampuni pinzani ya Linux ili kukuza mradi wake wa Azure Cloud kuwa na huduma nyingi za bure na wazi.

microsoft-loves-linux-azure-cloud

Linux imejizolea umaarufu mkubwa sana miongoni mwa mashabiki wa software kwa miradi yake mingi ya bure na ya wazi (Open Source Projects) kama mifumo endeshi yake ya Ubuntu, Fedora, Linux Mint na mingine mingi tu.

Katika miezi ya hivi karibuni tumeona mahusiano ya kibiashara kati ya Microsoft na Linux kama yanaanza kuimarika hasa baada ya Microsoft kuruhusu Ubuntu ndani ya Windows 10, kutoa Visual Studio ya bure kwa watumiaji wa Linux na mengine mengi.

Hali inaonekana kutengemaa zaidi kwani kwa mujibu wa vyanzo vingi duniani vinavyojihusisha na masuala ya teknolojia, kampuni hiyo hivi sasa inaajiri wataalamu wengi kutoka katika kampuni ya Linux ili kuimarisha mradi wake wa Azure.

Taarifa nyingine kutoka katika mtandao wa The Register zinasema Microsoft wanaingia mikataba na wafanyakazi wengi wa Linux maarufu kama penguinistas ili kutengeneza software za bure zitakazokuwa zinapatikana katika huduma yao hiyo ya Azure.

Katika kuongeza kikosi chake Microsoft pia waliungana na Mr. Linux, Wim Coekaerts aliyeibadilisha kampuni ya Oracle kuwa kampuni inayotengeneza bidhaa za Linux zaidi.

Mradi wa Azure ni mpango maalumu wa Microsoft kuleta huduma za bure na wazi ili kupunguza upinzani mkali unaoletwa na Linux katika soko.