Wataalamu wa mambo ya anga kutoka shirika la anga la Marekani NASA wametumia muda wao wa siku za mwisho wa wiki kutengeneza filamu inayoelezea dunia wakiwa katika kituo cha anga cha kimataifa.

NASA-astronauts-directors

Filamu hiyo inayotarajiwa kutoka April 29, imetengenezwa angani kwa kutumia muda wa ziada wa wanaanga hao ambao ni siku za mwishoni mwa juma na muda wao wa mapunziko. Wanaanga hao Kjell Lindgren, Terry Virts, na Barry Wilmore  wakiongozwa na Scott Kelly  wametengeneza filamu hiyo kwa ushirikiano na kampuni inayotengeneza kamera ya IMAX.

Walichaguliwa na kupewa mafunzo maalumu kabla ya kwenda katika Kituo hicho cha anga cha kimataifa (Internation Space Station) ili kutengeneza filamu itakayokuwa ikielezea hali ya dunia kwa sasa na viumbe vinavyoishi humo kutokea angani.

Ilichukua miaka mitatu kutafuta kamera gani inaweza kufanya kazi vizuri kutengenezea filamu hiyo huko angani kama anavyoeleza mmoja wa wanaanga hao. Filamu hiyo imeongezewa utamu na sauti ya mwanamama Jennifer Lawrence aliyekuwa muigizaji maarufu.