Unachukuzwa na harufu ya ngozi yako? Je, unahitaji mtu wa kukuambia kama unanuka au unanukia? Ondoa shaka, kampuni ya Nivea wametengeneza application inayoitwa NOSE itakayokuwezesha kujua hali ya harufu ya ngozi yako.

nivea

Kwa mujibu wa kampuni hiyo, wanaume wengi huwa hawajali sana kuhusiana na hali ya harufu ya ngozi zao, wengi wao huwa hawafahamu muda gani wananukia vizuri na muda gani huwa wanatoa harufu mbaya kwa sababu ni ngumu kwa mtu kufahamu harufu ya jasho lake kutokana na mazoea ya pua.

NOSE, imetengenezwa kwa msaada mkubwa wa kampuni ya Hppiness FCB, inafanya kazi kwa kusaidiana na sensa maalumu zinazowekwa katika kava la simu ili kuweza kugundua harufu ya mtumiaji kama ananukia au la.

Toleo la kwanza la application hii limefanyiwa majaribio nchini Ubelgiji na linatarajiwa kufanyiwa majaribio zaidi kabla ya kuingia sokoni.