Hapo juzi kampuni maarufu ya kutengeneza magari ya kifahari ya Mercedes-Benz ilialika waandishi wa habari kusini mwa Ufaransa kushuhudia boti ya kwanza iliyotengenezwa na kampuni hiyo.

mercedes-luxury-yacht

Boti hiyo imepewa jina la Mercedes-Benz Arrow460-Granturismo ni boti ya kipekee kabisa kuwahi kutokea baharini kwani ina kila aina ya starehe. Mercedes Arrow ina uwezo wa kubeba watu 10, imefuata nyayo za bidhaa nyingine zote kutoka kampuni ya Mercedes kwa kuwa na umbo zuri, huduma nzuri zitakazomwezesha mtumiaji kufurahia safari yake baharini.

Hata hivyo kwa sasa kampuni hiyo inadai itatengeneza boti 10 tu za mwanzo na moja ndio itauzwa nchi yoyote duniani kwa kiasi cha dola milioni 1.7 za kimarekani sawa na shilingi bilioni 3.7 za kitanzania.

Boti hiyo yenye urefu wa mita 14 inasukumwa na injini za dizeli au ya 480 HP Yanmar na ina uwezo wa kubadilika mwonekano kulingana na matakwa ya mtumiaji kwa wakati huo.

sailing-boat-across-water

merceded-best-yacht-custom