Simu ya kwanza ya Android kutoka kampuni ya Blackberry, Blackberry Priv inatarajiwa kupokea update ya Android Marshmallow kuanzia tarehe 3 May.

BlackBerry-Priv-review-keyboard

Simu hiyo iliyobadilisha mtazamo wa wengi wa mashabiki wa simu za Backberry kwa kuwa na mfumo endeshi wa Android itapokea pia update ya keyboard yake ya vitufe halisi ukiacha zile zilizozoeleka na wengi za kugusa kwenye kioo. Kutakuwa na zaidi za emoji 200 na watumiaji wataweza kuandika kwa kutelezesha vidole vyao kutoka herufi moja kwenda nyingine ili kuunda neno (Swipe).

Ikiwa na Marshmallow Blackberry Priv itapata pia;

  1. App Permission – Unaweza ukaruhusu app gani itumie nini
  2. App Standby – App zinazoendelea kufanya kazi kwa nyuma zitazimwa ili kupunguza matumizi ya battery
  3. Uwezo wa kurekodi video kwa slow motion na mwendo wa kawaida wa 24fps
  4. Uwezo wa kuencrypt media card
  5. Taarifa za kiusalama kama simu yako inadukuliwa au kama kuna mdudu ameingia