Kila siku ndege zinazidi kuongezwa ukubwa kulingana na mahitaji ya binadamu, hii imepelekea kampuni ya GE kutengeneza injini kubwa zaidi ya ndege yenye upana wa futi 11 kwa ajili ya ndege kubwa.

test-rig-jet-engine

Injini hiyo ya GE9X ndio injini kubwa zaidi kuwahi kutengenezwa katika historia ya ndege duniani na sehemu kubwa ya injini hiyo imetengenezwa kwa kutumia teknolojia ya 3D Printing. GE9X ilipelekwa katika eneo a majaribio ili kufanyiwa majaribio ya kwanza, unaweza ukaangalia video hapo chini kuona jinsi injini hii ilivyokuwa kubwa.