Uwepo wa Facebook, Messenger, instagram, Whatsapp na Pinterest kumeifanya App ya twitter ionekane sio kitu kwenye store hiyo na kuwafanya wamiliki wa app hiyo kuihamishia katika kipengere cha Habari (News).

Twitter-feed

Twitter imeamua kufanya hivyo ili kuepuka ushindani katika kipengere cha Social Network ambacho kimetawaliwa na Facebook, Whatsapp, Instagram, Messenger, Pinterest na nyingine nyingi na kuifanya twitter ishike nafasi ya kumi katika orodha hiyo.

Uhamisho huo unaonekana umeleta mafanikio kwani kwa sasa application ya twitter inashika nafasi ya kwanza katika orodha ya application za bure katika kipengere cha habari.

Kwa sasa mtandao huo wa kijamii unasuasua ukilinganisha na mpinzani wake Facebook, Twitter ina watumiaji milioni 310 kila mwezi, wakati Facebook ina watumiaji zaidi ya bilioni 1.6 kila mwezi duniani kote.