Eshima Ohashi Bridge,  kama linavyofahamika ni daraja lililopo nchini Japan katika eneo la Chukogu huko Honshu. Kwa sasa linashikilia rekodi ya daraja lenye mwinuko mkali zaidi linalotumiwa na magari huko nchini Japan.

eshima-ohashi-bridge
Picha kutoka imgur.com

Nchini kwetu tuna baadhi ya madaraja ambayo yamejizolea umaarufu kutokana na jinsi yalivyo ya kipekee, mfano mzuri ni daraja la Kigamboni (Nyerere Bridge), daraja la Mkapa pamoja na lile la Msimbati (daraja la Umoja). Huko Japan hali ni tofauti kidogo kwa sababu kuna kila aina ya madaraja marefu, lakini hili la Eshima Ohashi limetia fola kidogo.

steep-bridge-in-japan

Likiwa na mwinuko (slope) wa 6.1% daraja hili imekuwa likiwatisha sana madereva hasa kutokana na mwinuko wake mkali katika kupanda na kushuka darajani linashikilia rekodi ya kuwa daraja la tatu ukubwa la zege (rigid frame) duniani kwa mujibu wa NY Daily News.

eshima-ohashi-bridge-slope