Kuvuja kwa vyungu vya Nyuklia katika eneo la Fukushima huko Japan mwaka 2011 kulikosababishwa na tetemeko la ardhi na Tsunami ndio janga kubwa zaidi la kinyuklia kuwahi kuikuta dunia tangu kutokea kwa janga la Chernobyl 1986.

fukushima-2015-01

Baada ya wataalamu wa mambo ya nyuklia kupima kiwango cha mionzi katika mji huo kuna eneo la takribani maili 12.5 lililotengwa kutokana kuwa na mionzi mikali ya kinyuklia. Baada ya miaka minne ya eneo kukaa bila kuguswa na binadamu, miti na mimea mingine imeanza kuota na kufanya eneo hilo kuwa la mchanganyiko wa misitu, rami pamoja na majumba.

fukushima-201-02
Magari yaliyoachwa katika eneo hilo yamemezwa na msitu mnene wa miti na majani
fukushima-2015-03
Pikipiki iliyoachwa na mwenyewe ikiwa imefungwa kwenye nguzo dakika chache kabla ya tsunami
fukushima-2015-04
Magari ya michezo katika sehemu za starehe yalivyoachwa kabla ya tukio
fukushima-2015-05
Mpiga picha Arkandiusz Podniesinski akionyesha kiwango cha 6.7 uSv/h cha mionzi hiyo hatari katika eneo lililotengwa

 

Mifuko iliyojaa udongo ulioathiriwa na mionzi
Mifuko iliyojaa udongo ulioathiriwa na mionzi
Wataalamu wa mambo ya nyuklia wakikagua nyumba kuona kama itafaa tena kwa makazi
Wataalamu wa mambo ya nyuklia wakikagua nyumba kuona kama itafaa tena kwa makazi

Picha zote kwa hisani ya daily maily