Hakimu mmoja nchini Brazil amefunga mawasiliano kwa njia ya mtandao wa kuchat wa Whatsapp unaomilikiwa na Facebook kwa saa 72.

whatsapp

Kwa mujibu wa hakimu huyo wa kibrazil, Marcel Montalvao mtandao huo umeshindwa kutoa msaada wa taarifa za kesi za dawa za kulevya pale ulipoombwa kufanya hivyo.

Mwezi Machi, Montalvao aliamuru kukamatwa kwa afisa mwandamizi wa Facebook katika nchi za Kilatini bwana Diego Dzoran baada ya kukataa kutoa ushirikiano katika uchunguzi dhidi ya dawa za kulevya.

Whatsapp mtandao unaomilikiwa na Facebook umesema umekatishwa tamaa na kitendo hicho kwa kuwa wamekuwa wakitoa ushirikiano wa kutosha mahakamani.

Mtandao huo umekuwa ukifungiwa mara kadhaa nchini Brazil kwa miezi michache ya karibuni kwa sababu zinazofanana na hizo.

Chanzo: BBC