Kampuni ya kimarekani ya kutengeneza magari yanayotumia umeme ili kupunguza uchafuzi wa mazingira imedhamilia kutengeneza magari zaidi ya 500,000 ya umeme katika mwaka 2018.

tesla

Magari hayo aina ya Tesla Model 3 yatakuwa yamevuka lengo la miaka mitatu lililowekwa na kampuni hiyo hapo awali.

Kampuni hiyo ya Tesla ambayo kwa sasa ina matoleo mawili sokoni ya Model S sedan na magari ya michezo ya Model X sport utility imepania kuwa moja ya makampuni makubwa ya kutengeneza magari ifikapo mwaka 2018.

Kampuni ya Tesla inayomilikiwa na Elon Musk, inaungwa mkono na wanaharakati wengi wa mazingira duniani kwa magari yake hayo yanayopunguza kwa kiasi kikubwa uchafuzi wa mazingira.