Microsoft wametangaza hapo jana kuwa zaidi ya vifaa milioni 300 duniani kote vinatimia Windows 10.  Vifaa kama laptops, desktops, simu na x-box na zaidi vimetajwa kutumia mfumo endeshi huo mpya kutoka Microsoft.

windows-10

“Tunaona watu maofisini, mashuleni, nyumbani, kwenye biashara ndogo ndogo mpaka makampuni mkubwa wakihamia kwenye Windows 10 kwa kasi zaidi ya ilivyokuwa hapo awali, na wakitumia Windows 10 zaidi.” Alisema bwana Yusuph Mehdi, makamu wa rais mwenza wa kampuni ya Microsoft’s Windows na Devices Group katika post ya blog.

Kasi hiyo ya watu kuhamia Windows 10 imeongezeka ikiwa ni matokeo ya Microsoft kuamua kuachia upgrade ya toeo hilo bure mpaka kufikia July 29.

Baada ya July 29, Windows 10 itakuja ikiwa tayari ndani ya kompyuta mpya au mtu kununua nakala yake binafsi kwa zaidi ya dola za kimarekani $119.

Microsoft wanalengo la kufikisha vifaa bilioni 1 vinavyotumia mfumo endeshi huo kufikia mwaka 2018 kama wapinzani wao Apple. Kampuni hiyo bado inasua sua katika mauzo ya simu zinazotumia mfumo endeshi wao wa Windows na inatarajiwa kuongeza juhudi zaidi mwaka huu.