Kama wewe ni mtumiaji wa Smartphone, Laptop, Desktop, Tablet au kifaa kingine chochote kinachokuunganisha kwenye mtandao ni lazima utakuwa ushawahi kutumia moja ya huduma kutoka Google.

google-internet

Ni swala lisilopingika kwa sasa kuwa kampuni ya Google inaendesha asilimia 70 ya maisha yetu ya kimtandao kwa sasa hasa kama wewe ni mwanafunzi, mfanyakazi au mfanyabiashara unayetumia mtandao katika kufanikisha mambo yako. Jaribu kufikiria kama Google isingekuwepo wewe mwanafunzi wa sasa unayechukua shahada au diploma yako maisha yangekuwaje.

Ni ukweli usiopingika kuwa huwezi kuepeka kabisa huduma kutoka google kwa sasa, ukikosa kutumia Google Search utatumia Google drive, Google Map, Google Docs, Google Wallet, You Tube au hata Smartphones ambazo zinatumia mfumo endeshi wa Android.

Hebu tuangalie huduma hizo;

Google Now – Msaidizi wako wa kidigitali kutoka Google

google-now

Google Now haikuwa maarufu hapo kabla, lakini kwa sasa imeibuka kuwa moja ya huduma za muhimu zaidi kwa baadhi ya watu. Google Now inakupa taarifa za vitu vyote vya msingi vilivyo karibu nawe kawe kama mgahawa, ATM, vituo vya mabasi, hali ya hewa na vingine vingi.

Google Maps

google-maps

Mimi kama mmoja ya watu wanaopenda kusafiri sidhani kama kuna anayejua umuhimu wa ramani kama mimi. Kuangalia umbali kutoka eneo ulipo na unapoenda, kuangalia foleni za barabarani, kupima muda kutoka eneo moja mpaka jingine hizo ni faida chache tu za google map.

Simu za Nexus

nexus-6p-300x200@2x

Uwepo wa simu za Google Nexus zinazozalishwa na makampuni tofauti kama LG,Huawei na HTC kunaifanya Google kuwa kampuni ya muhimu katika ulimwengu wa teknolojia. Simu hizi zinapatikana kwa bei rahisi ukilinganisha na huduma inazotoa kwa mtumiaji wake. Simu za Nexus zinaonyesha mulekeo wa Google katika miaka ijayo ndani ya teknolojia.

Android

Best-Emulator-For-Android-768x510

Nadhani kwa sasa mfumo huu endeshi kutoka Google ni huduma ya pili inayotumika zaidi duniani baada ya Google Search Engine.  Kuanzia kwenye smartphones, Tv, saa, Magari na vifaa vingine vingi vimekuwa vikitumia mfumo huu. Google ameleta mapinduzi makubwa sana katika soko la simu duniani kwa kutumia mfumo endeshi wa android. Mfumo endeshi huu hauna cha kusimulia kwa sababu takribani vifaa bilioni 1.3 duniani kote vinatumia mfumo huu.

Google Drive

pdf-image-to-text-google-drive-2

Huduma hii kutoka Google inapatikana moja kwa moja pale tu unapofungua barua pepe kutoka google. Ni huduma inayokupa hifadhi ya data zako mtandaoni. Unaweza ukaweka kila kitu unachojisikia na ukakifungua mahali popote na kifaa chochote chenye uwezo wa kufungua aina hiyo ya data. Kwa kuanzia Google inampa kila mtumiaji wa huduma za barua pepe GB 15 za bure za huduma hii, na zinaweza kuongezwa kwa kununua.

Google’s Productivity suite

Google wamepeleka mbali zaidi uwezo kutengeneza mafaili na makarabrasha tunayotumia kila siku. Kwa sasa huduma kama za Office, Spread sheet, Presentation na nyingine nyingi unazipata katika Google Docs hivyo kukuwezesha kurekebisha faili lako hata kama lipo mtandaoni au kuchapa document mpya huko huko mtandaoni.

Google Photos

google-photos-blunder

Hapa kwa wapenda picha ndipo mahali pao, Google Photos inakuwezesha kuhifadhi picha zako zote kutoka katika vifaa vyako tofauti katika sehemu moja. Pia Google Photos inakuwezesha kuweka kumbukumbuku nzuri ya picha zako kwa kuweka maeneo ambayo picha hizo zilipigwa. Kwa watumiaji wa android hakuna maalamiko tena ya kupoteza picha au kuhangaika kuhamisha picha.

Chromecast Audio

Kwa kutumia Chromecast audio, unaweza ukapiga mziki katika spika za nyumbani kwako kwa kutumia Wi-Fi. Unaweza ukapiga mziki kutoka katika kifaa chako chochote kile iwe simua u kompyuta katika spika za nyumabani bila waya.

YouTube

youtube

Nadhani hapa sina vingi vya kueleza kwa sababu kila mtu yupo na ufahamu kuhusu Youtube. Uwezo wa kupakia na kupakua video bure kutoka Youtube kunaifanya huduma hii kuwa na watumiaji zaidi ya bilioni 1.5 duniani kote kwa mwezi. Youtube ina mabilioni ya video yanayofurahisha, kufundisha au kukuburudisha. Matumizi ya TV yamepungua kwa kasi sana kwa sababu ya huduma kama hizi.

Project Fi

Hii sio maarufu sana katika nchi za kiafrika, huduma hii inamuwezesha mtumiaji wake kupiga simu, kutumia data na kutuma ujumbe mfupi wa maneno popote pale duniani. Tofauti ya huduma hii na huduma nyingine ni kulipia kile tu unachokitumia.

Google Search Engine – Hii ndio huduma bora zaidi ya zote kutoka Google

google-segn

Haihitaji maelezo mengi sana, kwakifupi hapa utapata kila kitu unachotafuta. Google Search Engine imewacha mbali sana Bing na Yahoo Search katika huduma zake.

Kuna huduma nyingine nyingi sana kutoka Google kama Google Play Store, Google Project Era, Google Music, Google Currency Converter, Google Translator, Gmail, Google Device Manager na nyingine nyingi.

Hivyo haina shaka kuwa Google imefanya kila kitu mtumiaji wa mtandao au wa teknlojia angependa kufanya kwa sasa.

Kama umependa makala hii tafadhali like page yetu ili uweze kupata habari moto moto zaidi za kiteknolijia kutoka katika kila kona ya ulimwengu.