Kampuni ya kutengeneza magari ya Uingereza ya Jaguar Land Rover ambayo kwa sasa inamilikiwa na Tata Motors imepanga kuachia simu yao ya kwanza mwaka 2017 itakayoendana na bidhaa zao za magari.

fields-land-rover-jaguar-waukesha-004

Kampuni hiyo inayofahamika kwa kutengeneza magari ya thamani kubwa duniani kama Range Rovers na Jaguar imeingia ubia na kampuni ya kutengeneza vifaa vya umeme ya Bullitt Group katika kufanikisha hilo.

Kwa mujibu wa Bullitt Group ubia huo ni mwanzo wa kuleta bidhaa nzuri na zenye ubora zitakazomfanya mtumiaji kuwa n uhuru wa kuvuka mipaka katika matumizi ya gari na simu.

Simu hiyo inatarajiwa kuzinduliwa mapema 2017 ikiwa na mipangilio maalum kwa ajili ya kumsaidia mmiliki wa magari yanayozalishwa na kampuni hiyo.