Samsung wameachia rasmi toleo la friji (jokofu) lenye Tv ya inchi 21.5 touch screen  likiwa na uwezo wa kuvinjari mtandaoni, kuonyesha muvi na kuonyesha tarehe za kuharibika kwa bidhaa zilizomo ndani yake.

Samsung-Family-Hub-Refrigerator

Friji hilo kwa mara ya kwanza limezinduliwa jijini Monaco linabadilisha kabisa sura na mwenekano wa majokofu ya sasa kwa kuongeza vionjo zaidi katika uundwaji wake. Likiwa na kioo kikubwa cha touch screen friji hilo litamuwezesha mtumiaji wake kuangalia muvi, kuvinjari mtandaoni na kuangalia vinywaji au vitu vilivyomo ndani ya friji hilo kabla ya kulifungua.

Samsung-Family-Hub-Refrigerator-02

Friji hilo ndani lina kamera mbili zinazopiga picha kila friji linapofungwa na kufunguliwa na kutunza picha hizo kwa ajili ya usalama wa bidhaa zilizomo ndani ya jokofu hilo kupitia app maalumu.

Friji hilo pia lina uwezo wa kutunza kumbukumbu zote za muhimu kama kiasi cha jotoridi kilichomo ndani ya friji, mgandamizo pamoja na tarehe za kuharibika kwa bidhaa ndani zilizomo ndani.

Samsung-Family-Hub-Refrigerator-01