Watengenezaji wa kivinjari cha Opera (Opera Browser) wametoa toleo jipya la kivinjari hicho lenye huduma ya kupunguza matumizi ya betri mpaka asilimia 50 ukilinganisha na kivinjari cha Google Chrome kama wanavyoeleza.

opera-power-saving-mode

Opera wamefanya mabadiliko mengi katika kivinjari chao katika miezi ya hivi karibuni kama kuongeza huduma ya ad blocker na VPN katika kivinjari chake katika mwezi wa nne na kwa sasa wamekuja na huduma ya Low Power Mode.

Kivinjari hicho kitampa kiashiria mtumiaji wake kuwasha huduma ya Low Power Mode pale kiwango cha chaji katika betri lake kinapofikia asilimia 20.

Kwa mujibu wa opera kivinjari hicho kinafanya mambo yafuatayo ili kupunguza matumizi ya betri;

  • Kupunguza shughuli zilizo nyuma ya pazia
  • Kiasi kidogo cha maelekezo kinatumwa kwenda kwenye processor
  • Plug-ins zisizotumika huwa zinazimwa kwa muda
  • Inazima animation zote zinazopatikana katika tovuti mbali mbali
  • Inazima video zote unazoweza kuangalia mtandaoni
  • Inabadilisha theme (muonekano) wake ili kuendana na kiwango cha chaji kilichobaki.