Whatsapp, mtandao maarufu zaidi wa kuchat duniani umetoa rasmi application yao kwa ajili ya kompyuta za Windows na Mac OS ili kuwafikia watumiaji zaidi duniani.

whatsapp-desktop

Baada ya mwaka mmoja kupita tangu kampuni ya Whatsapp kuachia huduma ya Whatsapp Web, ambayo ilikuwa ikiwawezesha watumiaji kusoma na kutuma ujumbe kupitia katika vivinjari vyao vya kompyuta (Desktop Web Browsers) sasa kampuni hiyo imetoa application maalumu ya Whatsapp kwa kompyuta zinazotumia mfumo endeshi wa Windows na Mac OS.

Kwa sasa app hiyo inapatikana kwa watumiaji wa matoleo ya Windows kuanzia Windows 8 na kuendelea na watumiaji wa Mac OS kuanzia toleo namba 10.9 na kuendelea. Unaweza ukapakua (download) matoleo hayo hapa.

Application hiyo itafanya kazi sawa kama Whatsapp web kwani mtumiaji atatakiwa kuscan QR Code kutoka katika desktop app kwa kutumia simu yake ili aweze kutumia whatsapp. Kompyuta na simu vyote vitahitajika kuwa na internet.