Inaonekana siku si nyingi kampuni inayojihusisha na huduma za ujumbe mfupi ya Whatsapp itaachia huduma ya simu za video iliyosubiriwa kwa hamu na watumiaji wa mtandao huu kwa muda mrefu.

whatsapp-vide-call

Mpaka sasa kampuni hiyo haijaachia huduma hiyo katika mfumo endeshi wowote wa simu ila inasemekana hivi karibuni huduma hiyo itaanza kupatikana rasmi katika app hiyo.

Huduma hiyo kwa sasa inaonekana katika toleo la majaribio la app (beta version (v 2.16.80)) hiyo linalopatikana Play Store ya android. Utaweza kupata toleo hili kama tu umesaini makubaliana na whatsapp kwa kukubali kuwa mmoja ya watu wanaoweza kupakua toleo maalumu la majaribio. Unaweza kusaini hapa.

Katika toleo hilo inaonekana whatsapp hawajaweka kitufe maalumu kwa ajili ya video call ila ametumia kile kile cha call, baada ya kugusa hicho cha call sasa utaletewa machaguo mawili ya Audio Call au Video Call.