Kampuni ya Samsung imepanga kutoa matoleo 5 tofauti ya simu hizo katika kipindi cha mwaka 2016-2017 huku kivutio kikubwa kikiwa ni Galaxy X simu itakayokuja na kioo chenye uwezo wa kujikunja.

samsung-galaxy-x-foldable-phone

Utengenezaji wa simu hiyo umepewa jina la Project Valley na inatarajiwa kutoka mapema mwaka 2017 kama moja ya matoleo 5 yaliyopangwa kutolewa na kampuni hiyo.

Kadri siku zinavyokwenda makampuni ya simu yamekuwa yakitoa toleo jipya la simu kila mwaka ili kuendana na kasi ya soko linalokuwa kwa kasi hivi sasa. Kampuni ya Samsung inalitambua hilo na imepanga kuachia matoleo matano yanayotarajiwa kutikisa zaidi dunia kuanzia mwaka kesho.

Ripoti kutoka katika mtandao wa Sammobile zinasema toleo la Galaxy X litakuja na kioo cha 4K chenye uwezo wa kujikunja na kuwa kama wallet.

Hii ni orodha ya simu zinazotarajiwa kutolewa na kampuni hiyo hapo mwakani;

  • Samsung Galaxy X
  • Samsung Galaxy S8
  • Samsung Galaxy S8 Edge
  • Samsung Galaxy Note 7
  • Samsung Galaxy Note 7 Edge

Ripoti zinasema matoleo mengine yote tofauti na Galaxy X yatakuja na kioo cha QHD Super AMOLED .