Maelfu ya watu nchini Australia wanaopenda ndege walikusanyika kutizama ndege kubwa zaidi duniani ya Antonov An-225 Mriya, ilipowasili mjini Perth nchini humo.

antonov-landing

Ndege hiyo yenye urefu wa mita 84 na uzito wa tani 175 bila ya kubeba mzigo wala mafuta, ilikuwa ikisafirisha jenereta yenye uzito wa tani 117.

Misongamano ya magari ilifunga barabara wakati umati ulikusanyika kutizama kuwasili kwa ndege hiyo.

Ndege hiyo ilitoka mjini Prague na kusimama maeneo kadha mashariki ya kati na Asia, ikiwa safarini kwenda Australia.

Ndege hiyo kama inavyoonekana kwa mbele mara baada ya kuwasili nchini Australia
Ndege hiyo kama inavyoonekana kwa mbele mara baada ya kuwasili nchini Australia
Ndege hiyo ina jumla ya matairi 32 na injini kubwa 6
Ndege hiyo ina jumla ya matairi 32 na injini kubwa 6

Source: BBC