Kadri muda unavyozidi kwenda mahitaji ya maprograma wa kompyuta na simu yanaongezeka kwa kasi sana, asilimia 60% ya kazi zote za tech kwa sasa zinahitaji maprograma kwa mujibu wa Glassdoor.

lugha-9-za-kompyuta-01

Vijana wengi katika nchi zilizoendelea na hata zile zinazoendelea kwa sasa wanakimbilia masomo ya IT, Computer Science pamoja na Computer Engineering ili kuendana na kasi ya soko la ajira ambalo kwa sasa limegeukia upande huu. Moja ya kitu cha muhimu zaidi ni kujua kufanya kompyuta programing ambayo imekuwa ikiwasumbua watu wengi sana hasa katika fani hizi.

Siku hizi kuwa kompyuta programa sio lazima uwe mtu aliyesoma moja ya fani tajwa hapo juu, hapana unaweza ukajfunza programing hata kama wewe ni muhasibu, mwalimu au hata mtumishi wa kawaida wa serikali kama tu unamuda wa kutosha kufanya hivyo.

Hebu tuangalie orodha ya lugha 9 zinazobamba kwa sasa katika soko la ajira la maprograma kwa mujibu wa vyanzo mbali mbali;

lugha-9-za-kompyuta

1. SQL

Kama inavyotamkwa ‘sequel’ SQL ni kifupi cha Structured Query Language inashika nafasi ya kwanza kwa kuwa na matumizi makubwa zaidi duniani hasa katika mifumo yote inayohitaji database. Teknolojia za Database kama MySQL, PostgreSQL na Microsoft SQL Server zinatoa huduma katika maeneo yote ya muhimu kuanzia katika biashara ndogo mpaka kubwa, kwenye mahospitali, mabenki, vyuo na maeneo mengine mengi. Simu zote za Android na iPhone zina database ya SQLite na makampuni kama Google, Skype na Dropbox wanaituia moja kwa moja

2. Java

Hivi karibuni jumuiya ya maprograma walisheherekea miaka 20 ya Java. Java inatumika na zaidi ya maprograma milioni 9 na vifaa takribani bilioni 7 vinatumia lugha hii duniani kote kwa sasa. Java inatumika kutengeneza mfumo endeshi wa android hivyo unapata picha ni kwa jinsi gani lugha hii ilivyo na soko kwa sasa.

3. JavaScript

Hapa usichanganye JavaScript na Java. JavaScript ni lugha inayotumika zaidi katika masuala ya mtandao hasa katika Web-Programing. Kila kivinjari unachokiona kina sehemu kubwa ya lugha hii kama Mozilla Firefox, Google Chrome, Internet Explorer pamoja na Operamini.

4. C#

Lugha hii ilianzishwa katika miaka ya 2000 na kampuni ya Microsoft kwa ajili ya matumizi mbalimbali hasa katika bidhaa zinazotumia .Net Framework. Ni zao la lugha za C na C++ katika lugha nyepesi.

5. C++

Ikiwa imetambulishwa rasmi katika miaka ya 1983 na bwana Bjarne Stroustrup akiwa katika kampuni ya Bells Labs, C++ inabaki kuwa lugha pendwa kwa wataalamu wanaotengeneza magame hasa ya simu na kompyuta. Mifumo endeshi kama Microsoft na Mac OS kwa kiasi kikubwa hutumia lugha hii bila kusahau software kama Adobe.

6. Python

Haina muda mrefu sana tangu iingie katika mifumo ya elimu na baadhi ya makampuni makubwa kuamua kuanza kutumia lugha hii. Kwa sasa python inapendelewa zaidi na wanafunzi wapya wa mambo ya programing kwa sababu ya urahisi wake. PBS, NASA Reddit wanatumia lugha hii.

7. PHP

Ikiwa imetengenezwa na Rasmus Lerdorf mwenye asili ya Canada na Denmark mwaka 1994, haikuwa lugha ya kompyuta hapo kabla. Ilitengenezwa ikiwa ni kama mlolongo wa zana zinazomsaidia bwana Rasmus sawa Personal Home Page (PHP). Leo inafahamika kama (Hyper Text Pre-Processor)  PHP na inatumika katika upande wa Server na kwa kiasi kikubwa mitandao mingi inatumia lugha hii mfano mzuri ukiwa facebook.

8. Ruby

Ikiwa kama Java na C, Ruby ni lugha inayotumika katika vifaa tofauti tofauti japo inazidi kupoteza umaarufu kadri siku zinavyosonga.

9. iOS/Swift

Mwaka 2014, kampuni ya Apple waliamua kutengeneza lugha yao kwa ajili ya vifaa vyao vinavyotumia mifumo endeshi ya Mac OS na iOS. Kwa kiasi kikubwa lugha hii inafanana na C na Objective C.

Kabla ya kuchagua lugha gani ya kusoma ni bora ukafahamu kwa nini unataka kusoma lugha hiyo, ni vyema kuchagua lugha kulingana na mahitaji husika.