Wachina wameamua kuja na njia mbadala ya kupambana na foleni za barabarani kwa kuja na mradi mpya wa mabasi ya kisasa yenye uwezo wa kupita juu ya magari mengine bila shida.

Land-Airbus-TBS-China-1

Mabasi hayo marefu yatakuwa yakiendeshwa kwa nguvu za umeme na yatakuwa yana urefu wa mita nane kwenda juu ili kuruhusu mabasi hayo kuweza kupita juu ya magari mengine bila tabu.

Ndani ya mabasi hayo kutakuwa na kila aina ya huduma pamoja na zana za kisasa kabisa kama lift, mifumo ya kisasa ya breki zinazojibana zenyewe pale basi linapohisi hatari mbele.

Cheki hapa video inayoonyesha mradi huo.