Microsoft na Facebook wameungana ili kutengeneza mkondo mpya wa mtandao kwa kusambaza nyaya katika bahari ya Atlantic ili kuonganisha Marekani na Ulaya.

microsoft-230416

Makampuni hayo mawili makubwa yamesema yameungana ili kusaidia kuunda mkondo huo utakaosaidia kupitisha data za watumiaji wake wengi waliopo katika mabara hayo mawili.

Mradi huo utafanikishwa na kampuni ya kihispania ya Telefonica, ambayo itahusika moja kwa moja katika usambazaji wa mkondo huo na kuuza sehemu ya mkondo huo kwa makampuni mengine. Mkondo huo unatarajiwa kuunganisha Virginia na jiji la Bilbao huko Spain.

Makampuni ya Tech yamekuwa yakilipa fedha nyingi sana katika huduma ya mtandao kwa makampuni ya simu hivyo njia hiyo itapunguza gharama kwa Facebook na Microsoft. Hata hivyo FB na MS sio makampuni ya kwanza kufanya hivyo kwani Google tayari walishapitisha Cable katika bahari ya Pacific.