Kampuni ya Asus imeendelea kutoa bidhaa mpya katika mkutano wa kibiashara wa Computex unaofanyika huko Taipei kwa kuachia matoleo matatu makali ya Laptop ambayo ni Asus Transformer

3, Asus Transformer 3 Pro na ZenBook 3.

Asus Transformer 3 ni nyembamba na nyepesi sana huku ikiwa na upana wa 6.9mm, na kioo cha 12.6 inchi na mwanga wa nits 450 na kuifanya kuwa mashine nzuri kwa matumizi ya nje. Pia ina betri yenye uwezo wa kudumu kwa zaidi ya masaa 9 na keyboard ya kuchomoka .

Asus-Transformer-31
Asus Transformer 3

Transformer 3 Pro yenyewe ni nyembamba zaidi ikiwa na upana wa 8.35mm, kioo cha 12.6 kama Trasformer 3 na kamera ya mbele yenye uwezo wa 13MP huku ikipewa nguvu na processor kutoka intel familia ya Core i7 na RAM mpaka 16GB.

Asus-Transformer-3-pro-01
Asus Transformer 3 Pro

ZenBook 3 inaonekana imekuja kwa lengo maalumu la kupambana na MacBook kutoka Apple ikiwa na uzito wa kilo 2 tu. Inapewa nguvu na Processor ya Intel Core i7 na betri lenye uwezo wa kukaa na chaji mpaka masaa 9 kwa kuchajiwa mara moja.

Asus-Zenbook-31
Asus Zenbook 3