Ondoa background yoyote katika picha kwa kutumia simu yako ya android na kuifanya picha yako kuwa na mwonekano mzuri na wakuvutia kwa kuchagua nini kionekane nyuma ya picha yako.

Kuna muda unatamani picha uliopiga iwe na background (mzingira ya nyuma ya picha) tofauti na yale uliyopo. Mfano kuonekana kama upo kwenye mnara wa Parisi, beach au hata kwenye majiji makubwa duniani.

bg-eraser

Matumizi ya kuondoa background hayaishii hapo tu, kuna muda unaweza tengeneza passport size ya haraka kwa kutumia kamera ya simu yako na kuitumia kwa kuweka rangi ya background unayotaka kama ni blue, nyeupe au la.

Fuata hatua zifuatazo ili kuondoa background katika picha yako,

Hatua za kufuata ili kutoa bckground katika picha yako

1. Pakua na install app inayoitwa Background Eraser katika simu yako ya android.

2. Pale tu application inapomaliza kuinstall, ifungue na itakuonyesha machaguo yafuatayo. Chagua Load a Photo.

bge-1

3. Sasa chagua picha yoyote unayotaka kuondoa background na icrop katika eneo unalotaka litolewe background.

bge-2

4. Baada ya kucrop picha bonyeza Done

5. Sasa hapo utapewa machaguo matatu ya jinsi ya kuondoa background, auto, manual au eraser. Unashauriwa kuchagua auto huku ukiwa umezoom (kukuza) picha.

bge-3

6. Baada ya hapo sehemu kubwa ya background itakuwa imetoka, unaweza ukatumia eraser kusafisha baadhi ya maeneo ambayo hayasafishwa vizuri.

bge-4

7. Baada ya hapo bonyeza Done, alafu chagua smooth level to maximum ili kupata picha yenye mwonekano mzuri.

8. Mwisho kabisa bonyeza Finish, na hapo utakuwa tayari unapicha iliyotolewa background.

bge-4

Application hii inaptikana pia Google Play.