Kama hakuna mpangilio mzuri wa utendaji katika kutengeneza mobile app yoyote kiasi kikubwa cha fedha na muda vitatumika bila kufanikisha lengo. Kabla ya kuanza zoezi zima ni lazima ujue kukadiria kiasi gani cha muda, pesa na jitihada zinazohitajika ili kutengeneza app.

PROGRAMMING-APP-DEVELOPMENT-PROCESS

Wakati tunatumia App kama Whatsapp, Instagram au Facebook huwa hatufikirii ni kiasi gani cha pesa, muda na jitihada kimetumika katika kutengeneza App hizo. Makampuni yanayomiliki App hizo hutumia kiasi kikubwa cha fedha na muda katika kutengeneza na kumfanya mtumiaji asipate tabu kabisa.

Leo swahilitech tunakuletea maelezo katika picha ya jinsi zoezi zima la utengenezaji wa app linavyofanyika hasa tukiangalia zaidi upande wa pesa na muda. Samahani lugha ya kiingereza imetumika katika picha hii kwa sababu huwezi kuiepuka linapokuja suala zima la tecknolojia.

mobile-app-development-process-infographic