Mwanzoni mwa mwezi wanne kampuni ya simu ya Tecno ilitambulisha rasmi mfumo endeshi wa HiOs kwenye simu za J8 na C8 ambao ni mfumo endeshi unaofanya kazi juu ya Android uliotengenezwa na kampuni hiyo kwa ajili ya simu zake.

tecno-hiOS

Hata hivyo ni miezi miwili tu imepita na watu wengi wanaotumia mfumo huo wamelalamikia mapungufu mengi hivyo kuwafanya Tecno kutoa ufanunuzi juu ya hilo.

Katika forum ya Tecno inayojulikana kama Tecno Spot wamewaomba watumiaji wa mfumo endeshi huo kuwa wapole kwa sasa kwani wanashughulikia mapungufu hayo na hivi karibuni watatoa maboresho (update) mapya kwa ajili ya kurekebisha matatizo hayo.

Ifahamike kuwa sio Tecno tu wanaokumbwa na matatizo ya aina hii kwani hata Apple na Google huwa wanakumbwa na kadhia hii pale wanapotoa toleo jipya la mfumo endeshi.

Matatizo mengi ya mfumo endeshi huu yanaonekana kwa watumiaji wa simu za Tecno Camon C8 ambao waliupgrade kutoka katika Android Lollipop na kwenda kwenye Android Marshmallow HiOS version 1.0.

Hata hivyo tecno wametoa maelekezo kwa watumiaji wa simu za C8 jinsi ya kudowngrade simu hizo kurudi kwenye Android Lollipop kama ilivyo hapo awali.