Katika tukio la kustaajabisha, akaunti za twitter na pinterest za CEO wa Facebook bwana Mark Zuckerberg zimedukuliwa na kikundi cha wadukuzi kutoka Saudi Arabia. Cha kufurahisha zaidi kikundi hicho cha wadukuzi walionyesha password ya Zuckerberg ya mtandao wa LinkedIn ni ‘dadada’.

mark-zuckerberg-s-twitter-and-pinterest-accounts-hacked

Wakati mgunduzi wa mtandao wa Facebook bwana Mark Zuckerberg akiwa busy na mtandao wake wa Facebook, wadukuzi walikuwa busy kudukua akaunti zake za twitter na pinterest.

Wadukuzi hao kutoka Saudi Arabia inasemekana walitumia taarifa za kiusalama zilizovuja mtandaoni kutoka katika mtandao wa linkedin. Kikundi hicho kinachojiita OurMine Team kilidukua akaunti ya Zuckerberg mapema jumapili hii.